1. UTANGULIZI
A-hijra Islamic Primary School inamilikiwa na Taasisi ya ANSAAR MUSLIM YOUTH CENTER ambayo ina amini kuwa elimu ni jambo lenye umuhimu wa kwanza kwa Mwanadamu. Tunajifunza katika Qur’an kuwa Nabii Adamu (Alayhi ssalam) alielimishwa kwanza mazingira atakayoishi hapa duniani (Qur’an 2:31). Vilevile Mtume Muhammad (Swallallahu alayhi wasallam.) kabla ya kazi yake kubwa ya kuhuisha Uislam, alipewa amri ya kusoma kwanza (Qur’an 96:1-5).
2. LENGO LA SHULE NA MASOMO
Al-hijra Islamic Primary School ina malengo ya ujumla yafuatayo: -
-
Kuwaelimisha na kuwalea vijana wa Kiislam (kike na kiume) ili wawe Waislam na raia wema watakaotoa mchango mkubwa kwa Taifa na Ummah wa Kiislam kwa ujumla.
-
Kuwaandaa vijana wa Kiislam kuwa viongozi waadilifu wa kutegemewa na Taifa na jamii ya Kiislam kwa ujumla.
SEKULA
- Civic and moral education
- Kiswahili
- English language
- Mathematics
- Social studies and vocational skills
- Science and technology
DINI
- Tah-fidhil Qur’an
- Tarbiya
- Fiqhi
- Sira
- Tawhiid
- Hadithi
- Arabic language
- Adh-kar
3. MAENDELEO YA DARASANI
- Kila Mwanafunzi analazimika kufanya bidii katika masomo yote. Mwanafunzi mvivu hatavumiliwa
- Mwanafunzi wa darasa la tatu hadi darasa la sita hata ruhusiwa kuingia darasa linalofuata bila kupata wastani wa 31(B) au zaidi kutokana na mitihani yote aliyoifanya mwisho wa mwaka.
- Kujibidiisha katika kazi ni katika nidhamu ya Kiislam hivyo, kila Mwanafunzi atawajibika kushiriki kikamilifu katika kutenda kazi za usafi wa mazingira na kazi nyingine kama atakavyo elekezwa na Walimu au Viongozi wa Wanafunzi. Kutegea kazi ya darasani au nje ya darasa ni kukiuka maadili anayotarajiwa awe nayo Mwanafunzi wa Shule hii na Shule haitamvumilia.
4. SARE YA SHULE
Wanafunzi watakaodahiliwa shuleni hapa hawataruhusiwa kuja na nguo zaidi ya zitakazo ainishwa katika jedwali lifuatalo;